Wednesday, May 26, 2010

Uendeshaji pikipiki wadhuru afya ya watoto jijini Kisumu

Uendeshaji pikipiki  wadhuru afya ya watoto jijini Kisumu

Waendeshaji pikipiki jijini Kisumu wawangojea wateja. Ni mara nyingi waendeshaji pikipiki hawa hukosa adabu wanapokuwa kazini hasa wateja wanapokuwa wengi. Wengi wao huwabeba abiria zaidi ya mmoja kinyume cha sheria na tena huendeshasha vigari hivi bila ya kujali afya zao na zile za wateja wao. Picha na James Khalwale

Khalwale James
Ni jambo la kawaida tu kwa wanaoendesha pikipiki jijini kisumu kutovalia kofia yao rasmi yaani helmeti na nguo za kuzuia upepo mkali wanapokuwa kazini hata wakati wa vuli au masika. Wao huenda kwa kasi sana huku wakiyahatarisha maisha ya watu wengine wanaotumia barabara.

Hata ingawa tabia hii huwaweka hatarini kiafya, wadadizi kutoka pande zote mbili yaani wanaotumia pikipiki na maafisa wanaosisitiza sheria za trafiki wamelenga kuchukua hatua. Inashangaza kwamba pikipiki hizi hubeba abiria zaidi ya mmoja, wawili nyuma na mmoja(mtoto) mbele, kinyume na jinsi inavyotakikana. Mara nyingi, wao huwabeba watoto mbele ya vitufe vya kuingizia petroli karibu na vifua vyao.

Kwa hivyo, watoto huwazuia waendeshaji hawa dhidi ya upepo mkali, kazi inayofaa kuwa ya helmeti, buti na jaketi. Tabia hii hasa huonekana macheo na machweo watoto wanapopelekwa au kuotolewa shuleni.

Mwishowe, watoto watashikwa na magonjwa sugu hasa ya kifua na yale yanayoathiri njia ya kupumua kama vile Pneaumonia na asthma hasa tukizingatia umri wao ulio mdogo sana.

Walezi na wazazi wanafahamu athari zinazoambatana na matumizi ya pikipiki bila kutumia mavazi yafaayo.

Hivi maajuzi, maafisa wa polisi wa mrengo wa trafiki walipeksheni pikipiki na kuwanasa wahudumu wengi waliopatikana na hatia ya kutozingatia sheria za matumizi ya barabara.

“Peksheni dhidi ya pikipiki ni sawa tu na ile inayofanyiwa magari na sisi huangalia jinsi sheria za trafiki zinavyotumiwa na wahudumu. Tukishamaliza peksheni ya pikipiki, lengo letu kuu ni kupiga peksheni kwenye baiskeli na lori.” Alisema bwana Kinoti Martin, afisa wa udumishaji wa sheria za trafiki mkoa wa Nyanza wakati walipokuwa wanasaka mabasi yanayoendeshwa kinyume na kanuni hizo kule Ahero.

Ajali zinazohuzisha vyombo hivi vya matembezi zimeendelea kuongezeka hapa nchini. Katika maeneo ya Mashamba, watoto na watu wakongwe hujipata taabani na kuangua vilio pikipiki zinapokaribia kwa jinsi zinavyoendeshwa kwa mwendo wa kasi sana.

Siku chache zimepita sasa baada ya ajali mbaya zaidi baina ya pikipiki mbili zilizoonana uso kwa uso Kule Luanda. Watazamaji wa kisa hicho waliachwa vinywa wazi baada ya kutokuwa na uwezo wa kuwasaidia waathiriwa kwa maana walikufa papo hapo baada ya damu kutapakaa njiani na kuzuia biashara kwa muda mfupi.

Jambo linakera hata zaidi ni jinsi watoto wanavyohatarishiwa maisha yao ya baadaye. Jeneza la karibu zaidi na lililofiche ni kitufe hiki. Hata bila ya kutokea kwa ajali inayoonekana, hutayarisha kifo cha mtu yeyote anayekitumia bila ya kinga.

Kuakikisha matumizi bora ya chombo hiki bila kuhofia shida ya kiafya mhudumu anafaa kuzingatia maelezo haya.

Mafunzo ya uendeshaji
Waendeshaji wengi wa pikipiki Kenya hawajapata mafunzo rasmi ya kufanya kazi hiyo ndiposa mikasa mingi isiyopendeza kama iliyoonywesha hapa juu imemea mizizi. Kulingana na idara ya trafiki mjini Bungoma, ajali za pikipiki zimekuwa kero kubwa kabisa la maisha ya binadamu. Picha na James Khalwale.

Kwanza, madereva wengi humu nchini wamepuuza vyuo vinavyopeana masomo na ujuzi wa kuendesha na kupambana na hitilafu ya mitambo ya pikipiki. Wao hujifunza kuendesha pikipiki kutoka kwa wenzao vijijini na mitaani ambao walipitia hali ile ile.

Kwa sababu hii, wengi wao hawatambui sheria na nembo zinazotumiwa barabarani. Vile vile, hawana uwezo wa kujidhibiti vilivyo wanapoendesha pikipiki. Kwa mfano, wengi hawajui matumizi ya gia.

Matumizi ya madawa ya kulevya

Pili, Madawa ya kulevya ni hatari kwa kazi yoyote inayohitaji uangalivu wa hali ya juu. Mwenye kutumia madawa mara nyingi husahau maagizo na utaratibu unaohitajika hasa akiwa barabarani. Yeye hulegealegea hali inayoongeza uwezekano wa ajali ya aina yoyote.
Chunguza pikipiki yako kimakini

Kadhalika, kabla ya kuanza safari yoyote, chunguza ikiwa pikipiki ina hitilafu. Uchunguzi huu ni muhimu kwani utakuokoa dhiti ya breki kukataa, gurudumu kupungua hewa na kadhalika. Pikipiki siku hizi zimewekewa kioo rasmi cha kuzuia baridi kuingia kwenye kifua ingawa ni za bei ghali. Kioo hiki kikiwa dhabiti, utahakikishiwa afya bora.

Kuhakikisha unazingatia wengine wanaotumia barabara, vioo viangaza nyuma sharti viwe sawa. Taa zinazopeana ishara ya kila aina tena lazima ziwe kamili. Hali hii itazuia ajali nyingi za barabarani.
Mavazi.

Aidha, magonjwa ya kichwa yanaweza kukushika usipotumia kofya au helmeti na Mavazi mengine rasmi kama vile buti na jaketi. Wakenya wengi huendesha pikipiki huku wamevalia shati, slipasi na wengine hata na suruali fupi, pia kaptura. Mavazi haya ni sawa kwa wahudumu wa bodaboda ya baiskeli kwa sababu wao hutumia nguvu zao kuendesha kifaa hiki hali inayosababisha joto mwilini.

Pikipiki kwa upande mwingine hutumia mafuta ya petroli kuenda na miili yao haifanyi kazi. Hata kwa mwendo uliomdogo kabisa, kutovaa mavazi yaliyotajwa huathiri mwili kwa kiasi usichoweza kutambua haraka.

Magonjwa ya macho, kichwa, njia ya kupumua, ngozi ya mwili na kadhalika ni mojawapo tu ya madhara haya na matibabu yake ni ghali sana.

Je, unaonekana? Licha ya hayo yote, Kuendesha Pikipiki usiku kuna mahitaji mengi. Mhudumu sharti avae nguo inayorudisha mwangaza nyuma (reflector)ili kuzua ajali kutoka upande wa nyuma hasa kwa kugongwa na magari. Washa taa-ishara zinazotakikana ndiposa wengine wanaotumia njia wakuone. Honi haifai kutumiwa ovyo ovyo. Wakati mwingine polisi wa trafiki wananaweza kukushika kwa kuitumia vibaya au kufanya kelele zisizofaa.

Maagizo Zaidi Hatimaye, endesha polepole hasa kwenye kona au njia panda. Vilevile, kuna sehemu zilizo na ilani ya mwendo unaohitajika kwa mfano karibu na shule, sokoni na kadhalika.
Fanya uchunguzi wa macho kabla ya kutumia chombo kile. Ni hatia kwa watu wasioona vizuri kuendesha kitu chochote kwenye barabara iliyo na wahudumu wengi.

Usiendeshe karibu sana na magari na ujizuie kuwakasirikia dereva wengine kila maanake waweza kusababisha ajali kwa urahisi.

No comments:

Post a Comment